ST. MARY’S HOSTEL OF DODOMA

HISTORIA FUPI:

St. Mary’s Hostel ilianzishwa na Umoja wa wamama wakuu Tanzania –RWSAT (Religious Women Superiours’ Association of Tanzania}. Kwa sasa TCAS (Tanzania Catholic Association of Sisters). Wakati huo, St. Mary’s Hostel ilikuwa ikisimamiwa na Sr. Lambertha wa shirika la Devine Providence, aliyekuwa katibu wa wamama wakuu, chini ya uongozi wa Askofu Mathias Isuja Joseph wa Jimbo Katoliki la Dodoma (kwa sasa ni mstaafu).

20140516_145312
MHASHAMU BABA ASK0FU MSTAAFU MATHIAS ISUJA JOSEPH WA JIMBO LADODOMA (BABU)

Katibu huyo, mwanzoni alinunua jengo moja lenye ghorofa moja. Alipoondoka Sr. Lambertha, uongozi wa wamama wakuu uliwaomba masista wa Mt. Gemma wa Dodoma kusimamia Hostel hiyo. Utume huu ni kati ya kazi za kijamii wafanyazo watawa hao, ikiwa pia ni karama ya shirika lao, kuwapatia waschana malezi bora.

20140501_141506

Pia baadaye umoja wa wamama wakuu, ulinunua jengo lingine lenye ghorofa moja, lililo karibu na lile la kwanza.

20140501_140811

 

MALENGO YA HOSTEL

Malengo ya kuanzisha Hostel hii, kwanza kabisa ni kuwapatia wasichana wanaosoma sekondari, mahali pa kuishi kwa amani na utulivu ili wasome wakiwa katika hali ya usalama. Pia, kuwapa malei bora ya kukua kiroho, kimwili na kiakili, pia kuwasaidia kiasikolojia. Wasichana hao, wengi wao ni wale wanaotoka katika mazingira magumu, wanaotoka mbali na mji wa Dodoma na hawana ndugu karibu na shule wanazosoma. Wanaendelea kulelewa katika maadili mema ya kumcha Mungu, kuwa wabunifu, burudani, kuwaelimisha masuala mtambuka, kujijua na kuweka malengo katika maisha.

20140501_135950

Wengi wao walioishi St. Mary’s Hostel wamefanikiwa katika maisha, na wanaishi maisha ya kujitegemea wakiwa na amani na furaha katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Lengo la pili, ilikuwa kuwapatia wafanyakazi mahali pa kuishi, wale ambao hawana nyumba mjini Dodoma. Mchakato huo ulifanywa na Sr. Lambertha. Baadaye Hostel hiyo ilibaki kuwa ya wasichana peke yao.

20140501_140339 20140501_135833

 

MAHALI ILIPO

St. Mary’s Hostel ipo katikati ya mji, eneo la Uhindini – Dodoma. Mashariki toka Nyerere Squre, Magharibi toka Ofisi za Manispaa, Kaskazini toka Jamatini na Kusini toka Uwanja wa ndege.

Wasichana wa sekondari za Dodoma mjini wanaoishi mbali na shule zao, wanaakaribishwa.

20140501_141213

20140501_140635

MAWASILIANO

E-mail:

Simu:

Mob. 0755776867/0688012744

UONGOZI

Viongozi St. Mary’s Hostel tokea kuanza kwake ni kama ifuatavyo:

Sr. Lambertha, Sr [totop] to Top [/totop] Auziliatrce Njirani, Sr. Demira, Sr. Faustila, Sr. Irimina, Sr. Invilata Msuri, Sr. Monika Lukrensia, Sr. Inyasia Qasawa, Sr. Ponsiana P. Mataka, …..

Facebook Comments Box