Kwetu sisi wanadamu kifo ni fumbo wala hakuna hata moja atafutaye kufa wala kwa ugonjwa wala kwa lo lote. Kifo hakipokeleki. Kwa mwenye imani lakini, kifo ni uhamisho kwenda kwenye raha ya milele. Kubali usikubali.

Ndiyo!  Msomaji  wetu, tunahitaji daima kujipanga. Je niko tayari kulonga na Muumba wangu!    Mmmm!    Lazima kuamini makuu ya Mungu Inakuwakuwaje?   Kumkiri, kudumu katika imani  na kumpenda daima kwa matendo ya upendano …………..

Hata hivyo, Utukufu na Ukuu una Yeye hata milele na milele!!.  Amina.

Kwa unyenyekevu wote Baba Mwenyezi  uwasamehe, uwapokee kwako ndugu zetu  marehemu.   Pamoja nao,  Sr. Christiana,   Sr. Gemma,    Sr. Emidia,  Sr.  Calista,   Sr.  Patricia,  uliowachukua kwako karibuni, uwaachilie dhambi zao ili walitukuze jina lako pamoja na watakatifu wako mbinguni. Amina.

 

Asante  kwa upendo wako kwetu Mama Maria, tunawaleta kwako ndugu zetu marehemu wote, uwaombee msamaha na uwakabidhi kwa mwanao Yesu Kristu, katika utawala wake  mbinguni wamsifu pamoja na jeshi la watakatifu Amina.

 

Facebook Comments Box
Author